Kadi ya Uandishi wa Habari

Kitambulisho cha Uandishi wa Habari ni kitambulisho maalum kinachotolewa na Serikali kupitia Idara ya Habari-MAELEZO kwa mwandishi wa habari mwenye sifa za taaluma ya habari ili aweze kufanya kazi zake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zinazoongoza taaluma hiyo. Kitambulisho hiki hutolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 31 Desemba kila mwaka. Masharti: > Kuwa na cheti cha Stashahada na kuendelea cha Taaluma ya Uandishi wa Habari kutoka katika chuo kinachotambulika na Serikali.Kwa wahitimu wa vyuo vya nje ya nchi wanatakiwa kuthibitisha vyeti vyao katika Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU). > Kuwa na uzoefu wa miaka miwili na kuendelea kwa wenye elimu ngazi ya Stashahada ya Uandishi wa Habari > Picha tatu za pasipoti za sasa. > Kwa waandishi wa habari wa nje ya nchi maombi yao yanatakiwa kuambatana na Kibali cha Ukaazi wa nchi (Working Permit), Hati ya Kusafiria (Passport), Kitambulisho cha Uandishi wa Habari kutoka Taifa analotoka na kujaza Fomu maalum inayopitishwa na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania ya nchi anakotoka. Taratibu: > Jaza Fomu ya Maombi. > Wasilisha maombi kwenye ofisi ya Msajili wa Magazeti, Idara ya Habari-MAELEZO, S.L.P 8031, Dar es Salaam au kupitia baruapepe maelezo@habari.go.tz > Lipa kiwango cha ada kinachotakiwa, kwa waandishi wa habari wa ndani Tsh. 30,000/-, kwa waandishi wa habari wa nje Dola za Marekani 50 hadi Dola 1,000. Zingatia: > Jaza sehemu B ya Fomu ya Maombi iliyopitishwa na Mhariri au Mkuu wa Idara iliyoambatana na Muhuri wa Ofisi anayofanyia k