Namna ya kusajili Gazeti

Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) chini ya Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976, imetoa fursa kwa taasisi binafsi na zile za umma kusajili gazeti/jarida kwa lengo la kutangazahabari na taarifa zake kwa Umma. MASHARTI • Kuwa na katiba ya chama, kikundi, kampuni, shirika au taasisi. • Cheti cha usajili wa chama, kikundi, kampuni, shirika au taasisi. • Uthibitisho wa cheti cha kulipa kodi cha kampuni, chama, kikundi, shirika au taasisi binafsi. • Leseni ya Biashara ya kampuni, chama, kikundi, shirika au taasisi binafsi. • Wasifu binafsi wa wakurugenzi/wamiliki wa kampuni, chama, kikundi, shirika au taasisi binafsi. • Wasifu binafsi wa Mhariri, nakala ya cheti cha Shahada ya Taaluma ya Habari cha Mhariri na barua ya kukubali kuwa Mhariri wa gazeti/jarida husika. • Wasifu binafsi, nakala za vyeti vya taaluma za waandishi wa habari angalau wanne wa gazeti/ jarida husika. • Sera ya gazeti/jarida • Andiko la Mradi la uanzishaji wa gazeti • Mahali ofisi ilipo, anuani ya posta na namba ya simu • Uthibitisho wa uwezo wa kifedha wa kuchapisha matoleo 10 mfululizo (bank statement) • Muonekano wa jarida/gazeti • Ada ya usajili wa jarida/gazeti Tsh. 500,000 Taratibu • Andika barua ya maombi ya usajili wa gazeti/jarida inayoambatana na jina la gazeti/jarida unaloomba kusajili kwa Msajili wa Magazeti, Idara ya Habar-MAELEZO, S.L.P 8031, Dar es Salaam. • Jaza fomu ya maombi ya usajili wa jarida/gazeti. • Wasilisha fomu namba 3 ya usajili wa gazeti/ jarida kwa mchapishaji wa gazeti/jarida. ZINGATIA • Fomu namba 3 ya usajili wa gazeti/ jarida inayojazwa na mchapishaji wa gazeti/jarida inapaswa kugongwa muhuri wa wakili,hakimu wa mahakama ikiambatanishwa na stamp duty. • Fomu namba 4 ya wamiliki wa gazeti/jarida inapaswa kugongwa muhuri wa wakili, hakimu wa mahakama ikiambanishwa na stamp duty.