Maombi ya Ukumbi wa Mikutano

Idara ya Habari-MAELEZO inatoa huduma za Ukumbi kwa Wananchi, Taasisi za Umma na binafsi kwa ajili ya kuzungumza na Waandishi wa Habari ili kufikisha taarifa na habari zao kwa umma. Masharti > Kuwasilisha barua ya maombi ya ukumbi kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, S.L.P 8031, Dar es Salaam. > Kuwasilisha Taarifa utakayoitoa kwa waandishi wa habari kwa Afisa muhusika atakayesimamia mkutano huo kabla ya kuanza kwa mkutano. Taratibu: > Jaza hii hapa (Fomu ya Maombi). > Wasilisha maombi kwenye ofisi ya Mkurugenzi Idara ya Habari-MAELEZO, S.L.P 8031, Dar es Salaam. > Lipa kiwango cha ada ya ukumbi kinachotakiwa Tsh. 60,000 kwa saa Moja na Tsh. 120,000 kwa siku. Zingatia: > Kufanya BOOKING ya ukumbi siku mbili kabla ya mkutano.