Katibu Mkuu Wizara ya Habari Bibi.Suzan Mlawi aipokea Kilimanjaro Queens Jijini Dodoma.


Imewekwa 30th July, 2018

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Wanawake “Kilimanjaro Queens” imerejea nchini ikitokea Rwanda ilipokuwa ikishiriki mashindano ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama CECAFA ambapo imefanikiwa kutwaa Kombe la michuano hiyo.

Timu hiyo imepokelewa leo Jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi Suzan Mlawi ambaye mbali tu na kuipongeza timu hiyo lakini pia ameishukuru kwa kuipeperusha vyema Bendera ya nchi.

“Mmeiwakilisha vizuri nchi yetu mmeonyesha nidhamu na kubwa zaidi mmeshinda na kufanikiwa kutetea kombe lenu nawapongeza sana na nawaahidi Serikali itaendelea kushirikiana na nyie ili mlete mafanikio zaidi kwa nchi yetu”Alisema Bibi Suzan.

Aidha Bibi Suzan amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF ) kutafuta mikakati mizuri itakayosaidia timu hiyo kupata wadhamini kama zilivyo timu nyingine lakini pia kuandaa tuzo kwa wachezaji wanaofanya vizuri ili kutoa hamasa kwa wadau wengi kutoa ushirikiano wa kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Bw. Kidao Wilfred ameeleza kuwa mafanikio waliyopata Kilimanjaro Queens yametokana na ushirikiano mkubwa baina ya Serikali Jeshi la Kujenga Taifa, Benchi la ufundi pamoja na Taasisi yake kwa kuwa karibu, kuijenga na kuiandaa timu hiyo vizuri.

Naye kocha wa timu Bw.Bakari Shime amesema kuwa timu yake imefanya vizuri kutokana na kufuata maelekezo mazuri aliyowapa na wakayafuata, timu kucheza kwa weledi mkubwa pamoja na ushirikiano mzuri kwa wadau wa mpira wa miguu kwa wanawake.

“Vijana wamejituma sana wamekuwa na ari ya kutetea Kombe hili na kuhakikisha wanarudi nalo nyumbani na imekuwa hivyo,wamekuwa na nidhamu na wamesikiliza maelekezo tuliyowapa”Alisema Kocha Bakari Shime.

Timu ya Kilimanjaro Queens imetwaa ubingwa wa michu