Serikali kushirikiana na wadau mbalimbali kuhifadhi historia za Kiutamduni nchini.


Imewekwa 06th July, 2018

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali waliomstari wa mbele katika kuhifadhi historia ya Utamaduni wa Mtanzania ikwemo tamaduni za makabila.

Hayo ameyasema jana alipotembelea kituo cha Pembenne za Utamaduni kinachopatikana Hydom Mbulu Vijijini, ambacho kinahifadhi historia ya makabila manne ya Wadatoga, Wahadzabe, Waairaq na Wabantu.

“ Nimefurahishwa na hatua hii nzuri ya uhifadhi wa Utamaduni wa kabila zinazopatikana nchini mwetu, nasi kama Serikali tuanaahidi kushirikina nanyi kwa karibu kahakikisha kituo hiki kinatangazwa na kujulikana ndani na nje ya nchi kwa manufaa ya vizazi vilivyopo , vijavyo na wageni” amesema Mhe. Juliana Shonza

Aliongeza kwa kueleza ni vizuri sisi kama watanzania kuhakikisha tunalinda na kuhifadhi tamaduni mbalimbali kwa kuwa utambulisho wa jamii yeyote ile ni kupitia utamaduni wake.

Naye Afisa Miradi kutoka Pembenne za Utamaduni Bw. Nelson Faustine ameeleza kuwa kituo hicho kimekuwa ni kivutio kikubwa kwa wageni mbalimbali kutoka nje ,na kuiomba Serikali izidi kukitangaza ili kifahamike zaidi.

Katika ziara yake Naibu Waziri Mhe. Juliana Shonza aliweza pia kufungua mashindano ya Kombe la Mbunge (Flatei Cup) yaliyoandaliwa na Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay lengo ikiwa ni kuweka hamasa ya michezo kwa wananchi.

Mhe. Shonza aliigiza Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini Kuhakikisha inatenga maeneo ya michezo ili kukabiliana na changamoto iliyopo ya ukosefu wa viwanja.

“Sera ya michezo inasema kila Halmashauri inapopima viwanja lazima kuwe na mipango Miji kuhakikisha wanatenga maeneo ya michezo ili kuwapa fursa wanamichezo chipukizi kukuza vipaji vyao”amesema Mhe. Shonza

Kwa Upande wake Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay alisema ujio huo wa Naibu Waziri utawasadia kutatua changamoto mbalimbali za kimichezo ikiwemo ukosefu wa viwanja, vifaa vya michezo pamoja na walimu wa michezo.