Waziri Dkt. Mwakyembe aipongeza kwaya ya Furahini kuliombea taifa kudumisha amani.


Imewekwa 03rd October, 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameipongeza kwaya wa Furahini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Mijuhu Singida, Dayosisi ya Kati kwa uimbaji wao na kuliombea taifa kudumisha amani.

Dkt. Mwakyembe amesema hayo leo mjini Dodoma alipotembelewa na Uongozi wa kwaya wa Furahini kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) la Mijuhu Singida.

“Nchi inaongozwa kwa Baraka za Mungu, nanyi kama wanakwaya mnasaidia kuongoza nchi yetu kwa kuhamasisha wananchi na jamii kuitunza na kuisimamia amani yetu” Dkt. Mwakyembe.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kwaya wa Furahini Bw. Benjamini Ng’imba kwa niaba ya uongozi wa kwaya amesema kuwa wanaungana na Serikali kwa kuiombea nchi amani ili wananchi waendelee kufanya shughuli za maendeleo kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Aidha, Bw. Ng’imba ameongeza kuwa wamechukua fursa hiyo ya uimbaji kuuunga mkono juhudi za kudumisha amani na umoja miongoni mwa jamii kwa njia ya uimbaji kwa manufaa ya taifa pamoja na kizazi cha sasa na baadaye.