Waziri Dkt. Mwakyembe Azindua Kituo cha Radio Jamii cha TBC Jijini Arusha.


Imewekwa 12th March, 2018

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua kituo cha Redio Jamii cha TBC chenye masafa ya 92. 1 ambacho kimegharimu jumla ya milioni 627 leo Jijini Arusha.

Wakati wa uzinduzi huo Mhe. Dkt. Mwakyembe amesema lengo kuu la kuanzishwa kwa kituo hicho cha redio ni kuhabarisha umma wa Arusha na mikoa ya jirani fursa mbalimbali zinazopatikana katika Jiji hilo ukizingatia chanzo kikuu cha mapato yake yanatokana na Utalii wa ndani.

“Ni matarajioyangurediohiiitakuwamstariwambelekatikakutangazanakuelezafursambalimbalizinazopatikanakatikaJijila Arushapamojanakuhabarishaummamasualambalimbaliyakijamii,kisiasanakiuchumi” amesemaMhe.Dkt. Mwakyembe

Aidha ameeleza kuwa TBC kama Shirika la Umma halina budi kuhakikisha inatoa matangazo ya uhakika na ukweli kwa kuifikia jamii kubwa zaidi hususani zileza vijijini ambako vyombo vingine vya habari havijaweza kuwafikia.

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gabriel Daqarro ameushukuru uongozi wa TBC na Serikali kwa ujumla kwa kuona umuhimu wakuwepo kwa kituo cha redio jamii kwa ukanda wa kaskazini.

“Redio hii ya Jamii ni muhimu sana kwa watu wa Ukanda wa Kaskazini ukizingatia asilimia 80 ya mapato yake yanatokana na sekta ya utalii hivyo itatupa fursa ya kujitangaza zaidi” alisema Bw. Daqarro.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya TBC na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas ameeleza kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linahitajiuwekezajimkubwailikufikamaeneomengizaidinchini.

Vilevile Mkurugenzi Mkuu Shirika La Utangazaji La Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rioba amesema kuwa Redio jamii iliyofunguliwa rasmi leo Jijini Arusha ni mkakati wa Serikali kuwafikia wananchi wengi mahali popote walipo.