Habari

Dar es Salaam mwenyeji Michuano ya AFCON 2019.

Imewekwa : 5th Oct 2018

Serikali imesema Jiji la Dar es Salaam ndio litakalotumika katika mashindano ya AFCON mwakani kutokana na kuwa na miundombinu inakayokidhi mahitaji ya michuano hiyo.

Soma zaidi

Waziri Dkt. Mwakyembe awataka Waandishi wa Habari kuandika habari zenye utafiti wa kina.

Imewekwa : 4th Oct 2018

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa waandishi wa habari kujikita zaidi katika kuandika habari zenye utafiti wa kina ili kuhabarisha jamii kwa taarifa zenye kujenga uelewa mzuri zaidi.

Soma zaidi

Wadau wa Michezo Jitokezeni kuunga mkono timu ya Taifa-Dkt. Mwakyembe

Imewekwa : 4th Oct 2018

Wadau wa michezo jitokezeni kwa wingi kuiunga mkono timu ya Taifa kwa kununua tiketi za ndege kwa Dola za Kimarekani 1500 (sawa na 3.4 milioni) na Dola 2000 (sawa na 4.4 milioni) ili kushuhudia mechi baina ya Taifa Stars na Cape Verde Oktoba 12,2018.

Soma zaidi

Dkt. Mwakyembe: BMT waiteni TASWA kujadili Katiba kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Imewekwa : 3rd Oct 2018

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuitisha kikao na viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA) pamoja na baadhi ya waandishi wa habari hizo kujadili na kupitia katiba ya chama hicho.

Soma zaidi