Habari

Katibu Mkuu Wizara ya Habari afungua mdahalo wa Vijana kujadili hatma ya ajira kwa vijana nchini

Imewekwa : 19th Apr 2016

Vijana wametakiwa kugeuza changamoto kuwa fursa na kuwa na utamaduni wa kujiajiri na kuchapa kazi kwa bidii badala ya kusubiria kuajiriwa huku wakilaumu mamlaka zinazoshughulika na vijana nchini.

Soma zaidi

Waziri Nape avitaka vyama vya michezo kuimarishwa mikoani na wilayani

Imewekwa : 15th Apr 2016

Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo amewataka makatibu tawala wa mikoa na maafisa tawala wa wilaya kusimamia na  kuimarisha vyama vya michezo katika maeneo yao.

Waziri Nape ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Tabora na Singida ikiwa na nia yakutembelea maeneo yanayohusu sekta za wizara,kupokea taarifa ya mkoa na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari na mawasiliano wa mikoa husika.

“Tunalo tatizo la kuangalia vyama vya michezo katika ngazi ya Taifa peke yake,matokeo yake mikoani huku hali inakuwa mbaya na vyama vya michezo hivi  viangaliwe kwa upana wake na sio mpira wa miguu tu.”Alisema Waziri Nape.

Aidha waziri huyo mwenye dhamana ya michezo alisema kuwa mpira wa miguu umeingiliwa na wapiga dili kwani suala la rushwa kwa sasa limekithiri sana na hasa upangaji wa matokeo na hili linatokea hasa kwa kuwa vyama vya michezo ni legelege na hivyo wanatengenezwa watu wanajiita viongozi wa michezo kwenye mikoa na wilaya lakini ukweli wanatengenezwa wapiga kura wa kwenda kuwapigia kura wakubwa na wala hawana mpango na vyama vya michezo kwenye mikoa na wilaya zetu.

Pia waziri uyo amewaagiza makatibu tawala wa mikoa na maafisa tawala wa wilaya kuhakikisha wanavijua na pia kukutana na vyama vya michezo vya mikoa na wilaya zao ili kuhakikisha chaguzi zinafanyika kwani wao ndo walezi na wenyeviti wa kamati za maendeleo ya  michezo za wilaya na mikoa na ambae hatofanya hivyo atataftiwa kazi nyingine na kubainisha kuwa utawekwa utaratibu wa kuwakumbusha kwa maneno na kwa maandishi kwa namna hii tutafika mbali katika michezo nchini.

 

Soma zaidi

Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuandaa vipindi vya kuelimisha jamii na kujenga uzalendo

Imewekwa : 7th Apr 2016

Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kuandaa vipindi vya kuelimisha na kupunguza burudani kwa kuongeza idadi ya vipindi vya kujenga uzalendo, amani, mshikamano pamoja na umoja wa kitaifa

Soma zaidi

Maafisa utamaduni wametakiwa kushirikiana na wasanii kuboresha sanaa ili itumike kutangaza maeneo ya utalii wa utamaduni yaliyopo nchini

Imewekwa : 7th Apr 2016

Maafisa utamaduni nchini wametakiwa kushirikiana na wadau pamoja na kuandaa vikao vya mara kwa mara na wadau wa utamaduni wakiwemo wasanii ili kuweza kujenga ukaribu na kutoa elimu ya sanaa itakayosaidia kuboresha kazi za sanaa hivyo kutumia sanaa kutangaza maeneo ya utalii wa utamaduni yaliyopo nchini.

Soma zaidi