Habari

NAPE: ITUMIENI MICHEZO KUJENGA UZALENDO NDANI YA JESHI LETU

Imewekwa : 8th Apr 2016

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye amelihasa jeshi la wananchi wa Tanzania(JWTZ) kujenga uzalendo ndani ya jeshi letu kupitia michezo mbalimbali ndani ya jeshi hilo.

Waziri Nape ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya Ulingo wa Kisasa wa Ngumi kwa Jeshi hilo ili wautumie kwa ajili ya maandalizi mbalimbali ya mchezo wa ngumi kwani Serikali imeona ni sehemu salama Zaidi na nidhamu ya kuutunza ipo na hata pale utapoitajika kutumika kwingine uchukuliwe na kurudishwa jeshini hapo kwani jeshi hilo limeleta heshima kubwa ya michezo nchini na kulifanya baraza la michezo ya majeshi (BAMMATA) kuimarika zaidi.

“Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekuwa na mchango mkubwa sana katika michezo hapa nchini na limetuletea sifa kubwa sana kwetu na hivyo hatukuwa na shaka tulipoletewa ombi la ulingo huu.Ulingo huu  utumike vyema na ulete heshima hapa nchini”Alisema Nape.

Aidha Waziri nape alitoa rai kwa jeshi hilo kurudisha michezo jeshini kwani inajenga uzalendo na kuimarisha umoja,undugu na urafiki.Waziri huyo pia alikazia kuwa wizara yake itaendelea kushirikiana na jeshi hilo katika michezo mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Meja Jenerali Issa Nassor ambaye ni mkuu wa mafunzo na Operesheni Jeshini alimshukuru Waziri Nape na Wizara yake kwa kuwapa ulingo huo na kuwa utawasaidia sana katika suala la mazoezi na hata mashindano mbalimbali.

“Ulingo huo utatumika kwa mabondia wote Tanzania kwani utajenga Umoja na Kufahamiana na kukuza michezo na pia tutashirikisha askari wote kwani michezo ni sehemu ya kazi pia”.Alisema Meja Jenerali Issa.

Aidha alisema kuwa Msaada wa Ulingo huo ni chachu ya mazoezi na itawajengea wana mchezo huo chachu ya ushindi na kuwataka wadau mbalimbali wa michezo kuunga mkono jitihada za jeshi hilo kwani wana nia ya wazi ya kuwa kituo cha ubora.

Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo  imetoa ulingo huo kwa jeshi hilo baada ya kupewa msaada  na serikali ya watu wa china mwaka jana ikiwa ni jitihada za kuboresha michezo nchini.

 

 

 

 

 

Soma zaidi

Naibu Waziri Wambura aiagiza BMT kuongeza kasi ya kufuatilia viwanja vya michezo vilivyovamiwa

Imewekwa : 5th Apr 2016

BMT yaagizwa kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa viwanja vya michezo vilivyovamiwa nakuvirejesha kwa jamii kwa ajili ya matumizi ya michezo.

Soma zaidi

Nape awaasa kamati ya maudhui kuelimisha wadau wake

Imewekwa : 1st Apr 2016

Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Nnauye  amewaasa wajumbe wa kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kujenga mazoea ya kuelimisha Umma badala ya kusubiri makosa ili waweze kutoa adhabu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye alipokuwa akizindua kamati hiyo ya Maudhui leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Alisema ni vema kama wadau wakuu wakafahamu majukumu ya kamati hiyo na kuelimishwa nini wanachopaswa kukifanya ili kuzuia baadhi ya makosa ambayo yangeweza kuzuilika na kuongeza kuwa kinga ni bora kuliko tiba.

Katika uzinduzi wa kamati hiyo pia alitoa wito wa kuangalia jinsi ambavyo vyombo vya habari wanazingatia sheria ya matumizi ya asilimia sitini ya maudhui ya Kitanzania katika vipindi vyao kwani suala hilo bado lina lalamikiwa na wadau wengi.

“ Najua kuna ugumu wa kuisukuma hiyo sheria, ila isimamiwe vizuri,takwimu hazifurahishi sana na kama inaonekana sheria hiyo haitekelezeki ni bora iangaliwe kwa upya” alisema waziri.

Kwa upande wake mjumbe wa Kamati hiyo Bw. Joseph Mapunda alisema kuwa licha ya umakini watakao kuwa nao katika kutekeleza majukumu yao Kamati imedhamiria kuhakikisha inahamasisha suala la mafunzo kwa watangazaji yanatiliwa mkazo kwani watangazaji wengi hawana mafunzo bora ya utangazaji.

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya watangazaji  nchini wafanya kazi katika mazingira magumu inayopelekea utendaji usio na tija, hivyo kamati yao itafanya ushawishi kuhakikisha wanathaminiwa na kufanya kazi katika mazingira rafiki.

Soma zaidi

Waziri Nape awataka wauzaji wa Filamu za Nje kufuata sheria.

Imewekwa : 17th Mar 2016

Kufuatia kuwepo kwa Filamu nyingi za nje zinazouzwa hapa nchini  bila kufuata Sheria ya uuzaji wa kazi hizo Serikali imewataka wauzaji hao kufanya biashara hiyo kwa kufuata na kuzingatia sheria iliyowekwa ili kusaidia kukuza na kutangaza filamu za hapa nchini.

Soma zaidi