Habari

Naibu Waziri Wambura aiagiza BMT kuongeza kasi ya kufuatilia viwanja vya michezo vilivyovamiwa

Imewekwa : 5th Apr 2016

BMT yaagizwa kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa viwanja vya michezo vilivyovamiwa nakuvirejesha kwa jamii kwa ajili ya matumizi ya michezo.

Soma zaidi

Nape awaasa kamati ya maudhui kuelimisha wadau wake

Imewekwa : 1st Apr 2016

Waziri wa Habari,Sanaa, Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Nnauye  amewaasa wajumbe wa kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kujenga mazoea ya kuelimisha Umma badala ya kusubiri makosa ili waweze kutoa adhabu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye alipokuwa akizindua kamati hiyo ya Maudhui leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Alisema ni vema kama wadau wakuu wakafahamu majukumu ya kamati hiyo na kuelimishwa nini wanachopaswa kukifanya ili kuzuia baadhi ya makosa ambayo yangeweza kuzuilika na kuongeza kuwa kinga ni bora kuliko tiba.

Katika uzinduzi wa kamati hiyo pia alitoa wito wa kuangalia jinsi ambavyo vyombo vya habari wanazingatia sheria ya matumizi ya asilimia sitini ya maudhui ya Kitanzania katika vipindi vyao kwani suala hilo bado lina lalamikiwa na wadau wengi.

“ Najua kuna ugumu wa kuisukuma hiyo sheria, ila isimamiwe vizuri,takwimu hazifurahishi sana na kama inaonekana sheria hiyo haitekelezeki ni bora iangaliwe kwa upya” alisema waziri.

Kwa upande wake mjumbe wa Kamati hiyo Bw. Joseph Mapunda alisema kuwa licha ya umakini watakao kuwa nao katika kutekeleza majukumu yao Kamati imedhamiria kuhakikisha inahamasisha suala la mafunzo kwa watangazaji yanatiliwa mkazo kwani watangazaji wengi hawana mafunzo bora ya utangazaji.

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya watangazaji  nchini wafanya kazi katika mazingira magumu inayopelekea utendaji usio na tija, hivyo kamati yao itafanya ushawishi kuhakikisha wanathaminiwa na kufanya kazi katika mazingira rafiki.

Soma zaidi

Waziri Nape awataka wauzaji wa Filamu za Nje kufuata sheria.

Imewekwa : 17th Mar 2016

Kufuatia kuwepo kwa Filamu nyingi za nje zinazouzwa hapa nchini  bila kufuata Sheria ya uuzaji wa kazi hizo Serikali imewataka wauzaji hao kufanya biashara hiyo kwa kufuata na kuzingatia sheria iliyowekwa ili kusaidia kukuza na kutangaza filamu za hapa nchini.

Soma zaidi

BAKITA wahaswa kuhamasisha matumizi ya Lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi

Imewekwa : 10th Mar 2016

Watendaji Taasisi ya Kiswahili Taifa (BAKITA) wametakiwa kijitangaza na kushiriki katika matukio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kuhamasisha matumizi la lugha ya Kiswahili ili kiweze kufahamika na kutumika na mataifa mengine.

Soma zaidi