Habari

Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa watakiwa kuwa wabunifu


Vijana wameshauriwa kujali afya zao kwa kujiunga na Mfuko wa afya wa Jamii (CHF)

Imewekwa : 22nd Apr 2015

Vijana wameshauriwa kujiunga na Mfuko wa afya wa jamii (CHF) unaotoa huduma rafiki ya afya katika jamii ili kuweza kuwa na afya bora itakayopelekea kuleta uchumi imara ndani na nje ya jamii ya kimasai.

Soma zaidi

Miradi inayokopesheka chanzo cha kupata Mkopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana – Riwa

Imewekwa : 21st Apr 2015

Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kata za Monduli juu na Mfereji wametakiwa kuwa na miradi ya mfano inayokopesheka na inayoonekana ili kuweza kupata fedha zinazotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unaosimamiwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Soma zaidi

Fani za sanaa kutumika kuelimisha Umma Maudhui ya Katiba Pendekezwa

Imewekwa : 5th Mar 2015

Maafisa Utamaduni na wadau wa utamaduni wametakiwa kutumia sanaa kupitia fani mbalimbali kuhamasisha juhudi za kuifahamu na kuipokea katiba inayopendekezwa ili jamii ya watanzania kuweza kujipatia katiba inayokidhi mahitaji yao.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua kikao kazi cha kumi cha Sekta ya Utamaduni, Uwanja wa Taifa jana jijini Dar es Salaam.

Profesa Gabriel amesema kuwa lengo la kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni ni kutanabaisha maudhui ya Katiba inayopendekezwa hivyo kuwataka wadau wa utamaduni kutumia tasnia ya sanaa inayoumbwa na herufi K tatu zinazolenga Kuhabarisha, Kuelimisha na Kuburudisha jamii katika masuala mbalimbali.

“Utamaduni ni kama inta inayoshikamanisha watu, ni vyema wadau wa utamaduni mkatumia talanta mliyonayo kufikia fikra za watu kwani suala la katiba pendekezwa ni letu sote kama watanzania hivyo tujivunie kwa kuweka mambo kwenye vitendo na kuishi yale tunayoyasema” amesema Profesa Gabriel.

Naye Kaimu  Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bibi. Leah Kihimbi amesema kuwa sanaa imekua ikitumika kusaidia makundi mbalimbali katika jamii kutoa sauti zao kwenye mambo mbalimbali na kuamini kuwa sanaa ina nafasi kubwa ya kuhamasisha na kuelimisha jamii maudhui ya katiba inayopendekezwa.

Bibi. Kihindu amesema kuwa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kimewashirikisha maafisa utamaduni kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara kikiwa na madhumuni ya kueleza mchango wa fani za sanaa katika kuelimisha umma maudhui ya katiba inayopendekezwa na kutoa ufafanuzi wa masuala ya Sekta ya Utamaduni yaliyozingatiwa katika Katiba inayopendekezwa.

Akizungumza kwa niaba ya maafisa Utamaduni kutoka Halmashauri zote Tanzania Bara, Afisa Utamaduni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bw. Godfrey Msokwa amesema kuwa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kitawawezesha wadau wa utamaduni kutumia sanaa kuifikia jamii na kutekeleza maazimio yatakayokusudiwa na kikao hicho.

Kikao kazi cha 10 cha Sekta ya Utamaduni chenye kauli mbiu isemayo Fani za Sanaa zielimishe Umma Maudhui ya Katiba Pendekezwa kimelenga kutumia sanaa kama kichocheo na mbinu mojawapo ya kuelimisha, kuonya na kuelekeza mambo mbalimbali yanayoihusu jamii.

Soma zaidi