Habari

Fani za sanaa kutumika kuelimisha Umma Maudhui ya Katiba Pendekezwa

Imewekwa : 5th Mar 2015

Maafisa Utamaduni na wadau wa utamaduni wametakiwa kutumia sanaa kupitia fani mbalimbali kuhamasisha juhudi za kuifahamu na kuipokea katiba inayopendekezwa ili jamii ya watanzania kuweza kujipatia katiba inayokidhi mahitaji yao.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua kikao kazi cha kumi cha Sekta ya Utamaduni, Uwanja wa Taifa jana jijini Dar es Salaam.

Profesa Gabriel amesema kuwa lengo la kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni ni kutanabaisha maudhui ya Katiba inayopendekezwa hivyo kuwataka wadau wa utamaduni kutumia tasnia ya sanaa inayoumbwa na herufi K tatu zinazolenga Kuhabarisha, Kuelimisha na Kuburudisha jamii katika masuala mbalimbali.

“Utamaduni ni kama inta inayoshikamanisha watu, ni vyema wadau wa utamaduni mkatumia talanta mliyonayo kufikia fikra za watu kwani suala la katiba pendekezwa ni letu sote kama watanzania hivyo tujivunie kwa kuweka mambo kwenye vitendo na kuishi yale tunayoyasema” amesema Profesa Gabriel.

Naye Kaimu  Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Bibi. Leah Kihimbi amesema kuwa sanaa imekua ikitumika kusaidia makundi mbalimbali katika jamii kutoa sauti zao kwenye mambo mbalimbali na kuamini kuwa sanaa ina nafasi kubwa ya kuhamasisha na kuelimisha jamii maudhui ya katiba inayopendekezwa.

Bibi. Kihindu amesema kuwa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kimewashirikisha maafisa utamaduni kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara kikiwa na madhumuni ya kueleza mchango wa fani za sanaa katika kuelimisha umma maudhui ya katiba inayopendekezwa na kutoa ufafanuzi wa masuala ya Sekta ya Utamaduni yaliyozingatiwa katika Katiba inayopendekezwa.

Akizungumza kwa niaba ya maafisa Utamaduni kutoka Halmashauri zote Tanzania Bara, Afisa Utamaduni kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bw. Godfrey Msokwa amesema kuwa kikao kazi cha Sekta ya Utamaduni kitawawezesha wadau wa utamaduni kutumia sanaa kuifikia jamii na kutekeleza maazimio yatakayokusudiwa na kikao hicho.

Kikao kazi cha 10 cha Sekta ya Utamaduni chenye kauli mbiu isemayo Fani za Sanaa zielimishe Umma Maudhui ya Katiba Pendekezwa kimelenga kutumia sanaa kama kichocheo na mbinu mojawapo ya kuelimisha, kuonya na kuelekeza mambo mbalimbali yanayoihusu jamii.

Soma zaidi

Wasanii wa Filamu Nchini watakiwa kutokuwa makontena ya biashara haramu

Imewekwa : 18th Feb 2015

Wasanii wa Bongo Movie wameshauriwa kutumia taaluma waliyonayo kupanua wigo wa filamu nchini na kuitangaza Tanzania duniani kote kwa kuzingatia matumizi mazuri ya lugha ya Kiswahili katika filamu wanazozitengeneza.

Soma zaidi

Tanzania yaipongeza China kwa misaada ya kimaendeleo.

Imewekwa : 18th Feb 2015

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe, ameipongeza Serikali Jamhuri ya China kwa msaada wake wa kuhakikisha Tanzania imefungua idara ya maalum ya upasuaji wa moyo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

 
[removed][removed] [removed][removed] [removed][removed]

Soma zaidi

Halmashauri ya Wilaya ya Chunya yachangia Shilingi Milioni 210 katika Mfuko wa Vijana na Wanawake kwa kipindi cha miaka miwili.

Imewekwa : 25th Jan 2015

Halmashauri ya Wilaya ya Chunya iliyopo katika Mkoa wa Mbeya imefanikiwa kuchangia shilingi milioni 210 katika mfuko wa Vijana na wanawake kwa mwaka wa fedha 2013/2014 na 2014/2015.

Soma zaidi