Habari

Idara hii inasimamia na kuratibu shughuli za Serikali kwenye eneo la habari. Katika kutekeleza majukumu yake, Idara imegawanyika katika sehemu nne ambazo ni; Sehemu ya Ukusanyaji na Usambazaji wa Habari, Sehemu ya Uratibu wa Vyombo vya Habari, Sehemu ya Usajili wa Magazeti na Sehemu ya Mawasiliano Serikalini.

Majukumu ya Idara hii ni pamoja na;

• Kuratibu upatikanaji wa Habari kuhusu shughuli za Serikali na wadau wengine.

• Kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali

• Kuwa mamlaka ya Usajili wa Magazeti

• Kuratibu Vyombo vya Habari Nchini

• Kukusanya na kusambaza habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Serikali na kujibu hoja mbalimbali zinazojitokeza katika vyombo vya habari

• Kuendesha Tovuti ya Wananchi;