Sera na Mipango

IDARA YA SERA NA MIPANGO

1. UTANGULIZI

Idara ya Sera na Mipango inatekeleza majukumu yake kupitia Sehemu ya Sera, Sehemu ya Mipango na Bajeti na Sehemu ya Ufuatiliaji na Tathimini.

2. MAJUKUMU YA IDARA YA SERA NA MIPANGO

Kazi kuu ya Idara hii ni kuratibu shughuli zote zinazotekelezwa na Wizara. Aidha, Idara hii hutoa utaalamu na huduma kwa masuala ya utungaji, utekelezaji, kufuatilia na kutathmini Sera za Wizara. Vilevile, Idara hii ni kiunganishi kati ya Idara na Vitengo vyote Wizarani. Majukumu mengine ni pamoja na:

i Kuratibu utungaji wa Sera za Wizara, kufuatilia utekelezaji wake na kufanya tathimini;

ii Kuchambua nyaraka mbalimbali kutoka Asasi nyingine na kushauri juu ya nyaraka hizo;

iii) Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mipango na Bajeti ya Wizara;

iv) Kufanya Ufuatiliaji na Tathimini ya Mipango na Bajeti na kuandaa taarifa ya utekelezaji;

v Kufanya utafiti, tathimini ya mipango ya Wizara na kutoa uamuzi wa mwelekeo wa mbele wa Wizara;

vi Kumotisha na kuwezesha utoaji wa huduma kwa Wizara kwa kutumia sekta binafsi;

vii) Kuratibu maandalizi ya michango ya Hotuba za Bajeti na Taarifa za Uchumi za mwaka za Wizara;

viii) Kujenga uwezo wa Mpango Mkakati, Bajeti, Ufuatiliaji na Tathimini katika Wizara; na

ix Kuhakikisha kuwa Mipango na Bajeti za Wizara inajumuishwa katika Mipango na Bajeti za Serikali

3. UONGOZI NA UTAWALA

Idara ya Sera na Mipango inaongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango na kusaidiwa na Wakurugenzi Wasaidizi kwa kila sehemu.