Ukumbi wa Mikutano

KUPATA HUDUMA YA UKUMBI WA MIKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI

Idara ya Habari-MAELEZO inatoa huduma za Ukumbi kwa wananchi, taasisi za umma na binafsi kwa ajili ya kuzungumza na Waandishi wa Habari ili kufikisha taarifa na habari zao kwa umma.

Masharti

> Kuwasilisha barua ya maombi ya ukumbi kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, S.L.P 8031, Dar es Salaam.

> Kuwasilisha Taarifa utakayoitoa kwa waandishi wa habari kwa Afisa muhusika atakayesimamia mkutano huo kabla ya kuanza kwa mkutano.

Taratibu:

> Jaza hii hapa (Fomu ya Maombi).

> Wasilisha maombi kwenye ofisi ya Mkurugenzi Idara ya Habari-MAELEZO, S.L.P 8031, Dar es Salaam.

> Lipa kiwango cha ada ya ukumbi kinachotakiwa Tsh. 60,000 kwa saa Moja na Tsh. 120,000 kwa siku.


Zingatia:

> Kufanya BOOKING ya ukumbi siku mbili kabla ya mkutano.